• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: KRA yatoa onyo kwa wafanyibiashara kukwepa kulipa ushuru.

    (GMT+08:00) 2020-05-04 15:48:42

    Huku biashara nyingi nchini Kenya zikichukuwa mkondo wa kufanyia biashara zao mitandaoni, mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA, yametoa onyo kali kwa wale wote wenye nia ya kuhepa kulipa ushuru.

    KRA inasisitiza kwamba wafanyibiashara wote ambao wamepeleka biashara zao mitandaoni, wahakikishe kwamba wanalipa ushuru kulingana na sheria zilizopo.

    Njia ya biashara kwenye mitandao inaonekana kushika kasi nchini Kenya, huku pia maduka makuu yakifuata mkondo huo. Biashar hii ilipigwa jeki mwezi Machi mwaka huu, baada ya Benki kuu nchini kuweka mikakati ya kuwaraia wakenya kulipia bidhaa kwa njia ya simu badalaya pesa taslimu.

    Serikali imekuwa ikiwashauri wakenya kujiepusha na matumizi ya pesa taslimu kama njia moja ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako