• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Urejeshaji mikopo usimamishwe mara moja.

    (GMT+08:00) 2020-05-04 15:48:58

    Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) jiji la Dodoma, Ringo Iringo, ameishauri serikali kuzungumza na taasisi za Kifedha ambazo zimetoa mikopo kwa wafanyibiashara, kusimamisha ulipaji wa marejesho au kupunguza riba, kutokana na biashara kuathiriwa na ugonjwa wa corona.

    Iringo anasema mlipuko wa virusi vya corona, umeathiri wafanyibiashara wote,akibainisha kuwa hali inatishia hatma yao, kutokana na wengi wao kuendesha shughuli zao kwa mikopo, kutoka taasisi mbalimbali za kifedha.

    Mwenyekiti huyu anasisitiza kwamba ili kuwasaidia wafanyibiashara waliofunga biashara zao kutokana na kudorora kwa uchumi duniani kote, serikali haina budi kukutana na taasisi za kifedha nchini Tanzania, ili kuona namna bora ya kuwasaidia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako