• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Matumizi ya umeme yapungua kwa asilimia kumi

    (GMT+08:00) 2020-05-04 15:49:40

    Tangu kufungiwa kwa takriban shughuli zote nchini Uganda kwanzia mwezi Machi, matumizi ya nguvu za umeme yamepungua kwa asilimia kumi.

    Kwa mujibu wa kampuni ya kusambaza umeme nchini Uganda (UETCL), kumekuwepo na upungufu wa matumizi ya nguvu za umeme kutoka megawati 680 hadi megawati 600.

    Sababu ya upungufu huu ni kutokana na kufungwa kwa biashara nyingi ambazo huchangia pakubwa sana ukuaji wa sekta ya nguvu za umeme uganda.

    Viwanda ambavyo hutumia zaidi ya asilimia 60 ya nguvu za umeme za kitaifa vimepunguza kwa kiasi kikubwa sana shughuli zao kutokana na sheria iliyopo kwa sasa ya kuzuia mambukizi ya virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako