• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Miundo 15,000 ya jeni za virusi yaonyesha virusi vya Corona havikutengenezwa na binadamu

  (GMT+08:00) 2020-05-05 10:08:38

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Shirika la Afya Duniani WHO, mkurugenzi wa kiufundi wa Programu za Dharura za WHO Bibi Maria Van Kerkhove amesema virusi vya Corona vinaenea kati ya popo, hivi sasa miundo 15,000 kamili ya jeni za virusi unaonyesha kuwa virusi vya Corona havikutengenezwa na binadamu. Amesema WHO inashirikiana na FAO, Shirika la afya ya wanyama duniani na idara mbalimbali za China, kutafuta wanyama wanaobeba virusi vya Corona, ili kuepuka binadamu kuambukizwa tena virusi hivyo kutoka kwa wanyama.

  Mkurugenzi mkuu wa Programu za Dharura za WHO Bw. Michael Ryan amesema WHO haijapata ushahidi kuhusu kauli ya Marekani inayodai kuwa virusi vya Corona vilitoka taasisi ya utafiti wa virusi ya Wuhan. Kwa upande wa WHO, kauli hiyo ni ya kukisia. Amesisitiza kuwa maoni yote iliyopata WHO na ushahidi wa miundo ya jeni za virusi vyote vinaonyesha kuwa virusi vya Corona vinatoka mazingira ya asili.

  Bw. Ryan pia amesema vipimo vya virusi vya Corona havipaswi kuzingatia utajiri wa mtu na uwezo wa kumudu gharama. Amesema inapaswa kupima watu wote wanaohitaji kupimwa, hasa kwa wale wasio na mazingira ya kujitenga na wale walio hatarini zaidi kuambukizwa na kufa virusi hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako