• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Hatma ya Ligi Kuu Rwanda kujulikana wiki hii

    (GMT+08:00) 2020-05-06 15:45:52

    Shirikisho la Soka Rwanda limesema kuwa uamuzi wa hatma ya msimu wa Ligi Kuu ya Rwanda 2019/20 utajulikana wiki hii. Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Francois Regis Uwayezu amethibitisha taarifa hiyo, na kuongeza kuwa wanaangalia uwezekano mwingine, kwani lolote linawezekana. Ila ameweka wazi kuwa uamuzi wowote utakaofikiwa itazingatia mwongozo wa nchi hiyo katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Hatua hiyo inatokana na maelekezo kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa wanachama wake kuwa wanatakiwa kuamua kama ligi zao zitaendelea ama la kutokana na janga la virusi vya Corona. Ligi Kuu Rwanda na shughuli nyingine za michezo zilisimamishwa tangu Machi 15 ili kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako