• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: ZFF yaisikiliza serikali kuhusu Ligi Kuu Zanzibar

    (GMT+08:00) 2020-05-06 15:46:28

    Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Haji Issa Kidali amesema, kwa sasa wanasubiri mwongozo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kujua kama ligi zote zitaendelea ama la. Kidali amesema, matarajio yao ni ligi hizo kurejea tena dimbani kati ya mwanzo wa mwezi ujao, endapo tu serikali itatoa mwongozo wa kufanya hivyo. Amesema ana matumaini makubwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itatoa tamko juu ya kuchezwa ligi hiyo kuendana na hali itakavyokuwa. Alisema awali, Kamati ya Mashindano kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi, walikuwa na majadiliano mafupi juu ya hatma ya ligi hiyo ambayo imesimama kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako