• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari kavu kibaha kukamilika ndani ya miezi 2

    (GMT+08:00) 2020-05-06 19:50:18

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusidedit Kakoko, amesema utekelezaji wa mradi wa Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Kibaha mkoani Pwani, unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu.

    Kakoko alisema mradi huo utatekelezwa katika hekta 60 kati ya 500 za eneo lililotwaliwa na mamlaka hiyo katika Kata ya Kwala chini ya Mkandarasi Suma JKT kwa gharama ya Sh. bilioni 47.

    Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilihusisha ufyekaji wa eneo la hekta 120, usawazishaji, kujaza kifusi, matabaka ya changarawe na ujenzi wa reli wa kilomita 1.3 kutoka kituo cha Kwala hadi bandarini hapo.

    Awamu ya pili, alisema ilihusisha kunyanyua tuta, kumwaga zege na kuweka reli tano zenye urefu wa mita 500 na kuzungusha ukuta wenye urefu wa kilomita 3.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako