• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Benki kuu ya Rwanda yapunguza kiwango cha kukopesha hadi asilimia 4.5

    (GMT+08:00) 2020-05-06 19:51:33

    Benki kuu ya Rwanda imepunguza kiwango chake cha kukopesha hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia tano, ili kukuza uchumi wakati wa janga la corona ambalo limepunguza kasi ya shughuli za kiuchumi.

    Taarifa kutoka kwa benki kuu inasema uamuzi huo, pamoja na hatua zingine za sera zilizotekelezwa Machi, zitasaidia benki za biashara kuendelea kufadhili uchumi.

    Benki hiyo imesema Kamati ya Sera ya Fedha imekagua maendeleo hasi ya hivi karibuni ya kiuchumi kabla ya kufikia uamuzi wa kupunguza kiwango cha riba.

    Mfumuko wa bei nchini humo unakadiriwa kushuka katika nusu ya pili ya 2020, kutokana na kushuka kwa mahitaji ya jumla.

    Benki kuu imetoa wito pia kwa benku za kibiashara kurekebisha mikopo yake na kurahisisha masharti ili kuwezesha waliokop kulipa.

    Kufikia Aprili 10, benki za biashara zilikuwa zimerekebisha mikopo yenye thamani ya dola milioni 272.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako