• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Thiago Emiliano da Silva asema ubingwa wao ni mali ya madaktari dunia nzima wanaopambana na corona

    (GMT+08:00) 2020-05-07 08:47:35

    Nahodha wa PSG, Thiago Emiliano da Silva amesema kuwa wameshinda ubingwa wa maajabu ambao ni mali ya madaktari dunia nzima. PSG walitangazwa kuwa mabingwa wa Ufaransa, Ligue 1 baada ya ligi hiyo kushindwa kuendelea msimu huu kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona. Serikali ya Ufaransa imesema kuwa masuala ya michezo yataruhusiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu ambao ni muda wa maandalizi kwa ajili ya msimu ujao. Silva amesema kuwa ingawa ubingwa unabaki kuwa alama kubwa kwenye mafanikio yao lakini ni mali ya madaktari wote duniani ambao wanatumia nguvu kubwa kupambana na Virusi vya Corona. PSG imetwaa ubingwa baada ya kucheza mechi 27 ikiwa na pointi 68 na kuwaacha kwa pointi 12 wanaowafuta Marseille ambao wana pointi 56 baada ya kucheza mechi 28.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako