• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya bidhaa nje ya China yaongezeka kwa asilimia 8.2 mwezi Aprili

    (GMT+08:00) 2020-05-07 17:02:56

    Takwimu mpya zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China GACC zimeonesha kuwa, mauzo ya bidhaa nje ya China katika mwezi Aprili yaliongezeka kwa asilimia 8.2 kuliko mwezi Machi na kufikia dola za kimarekani trilioni 1.41, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiwango hicho kuwa chanya tangu mwaka huu uanze.

    Mkurugenzi wa idara ya takwimu na uchambuzi ya GACC Li Kuiwen amesema, hali hiyo imeonesha kuwa mwelekeo wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona umeimarishwa nchini China, shughuli za kazi na uzalishaji zinazidi kurejeshwa, na ufanisi wa kutuliza biashara ya China na nchi za nje umeonekana dhahiri.

    Hata hivyo, takwimu hizo zimeonesha kuwa uingizaji wa bidhaa kutoka nje nchini China katika mwezi Aprili ulishuka kwa asilimia 10.2 na kuwa dola za kimarekani trilioni 1.09, na kufanya biashara ya China na nje katika mwezi Aprili ishuke kwa asilimia 0.7 tu kuliko mwezi Machi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako