• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wachezaji wote LaLiga kufanyiwa vipimo, klabu zote kuanza mazoezi wiki hii

    (GMT+08:00) 2020-05-07 17:03:20

    Wizara ya Afya nchini Hispania imesema klabu za LaLiga zinarejea tena katika mazoezi wiki hii tangu kusimama kwa ligi hiyo kuepusha kuenea kwa virusi vya Corona. Kufuatia kurejea kwa mazoezi, LaLiga imeandaa taratibu maalumu za Kiafya ambazo zitafuatwa na wachezaji wote wa LaLiga Santander na LaLiga SmartBank kwa kufanyiwa vipimo vya Afya. Kuanza upya kwa mazoezi hayo ni mipango ambayo imepangwa na LaLiga huku kukiwa na makubaliano na mamlaka ya Afya ili kuhakikisha kila mmoja anabaki kuwa salama na mwenye afya. Katika hatua za awali wachezaji watafanya mazoezi mmoja mmoja wakati jaribio hilo litachukua takribani wiki nne huku wakifanyiwa vipimo kisha baada ya kuonekana kuwa kuna usalama wa kutosha basi watafanya kwa makundi kama ilivyozoeleka ambapo LaLiga ikitarajiwa kuanza kutimuwa vumbi mweji Juni. Kurudi kazini kwa wachezaji hao kutaenda sambamba na uokoaji wa sekta muhimu sana ya Kiuchumi ambayo inachukua asilimia 1.37 ya pato la Taifa la Uhispania na kutengeneza ajira 185,000. Huu ni wakati ambapo hali ya Uchumi wa nchi sasa utahusika baada kukabiliwa na janga kiafya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako