• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Uturuki: Tupo tayari kwa fainali Ligi ya Mabingwa

    (GMT+08:00) 2020-05-07 17:04:03

    Rais wa Chama cha Soka nchini Uturuki, Nihat Ozdemir amesema taifa hilo liko tayari kwa mchezo wa fainali Ligi ya Mabingwa barani Ulaya katika tarehe itakayopangwa ndani ya mwezi Agosti mwaka huu. Uwanja wa Atatürk Olympic uliopo katika jiji la Istanbul ndiyo uliopangwa kuamua fainali hiyo kabla ya michezo yote kusitishwa mwezi Machi kutokana na janga la virusi vya Corona. Nihat amesema ligi kuu ya nchi hiyo itaendelea kuanzia Juni 12 mwaka huu, lengo likiwa ni kumaliza michezo yote ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu. Tayari klabu za Paris Saint-Germain (Ufaransa), RB Leipzig (Ujerumani), Atalanta (Italia) na Atlético Madrid (Hispania) zimeshatinga hatua ya robo fainali, baada ya kushinda michezo ya hatua ya 16, kabla ya kusimamishwa kwa michiano hiyo mwezi Machi. Klabu ambazo zilitarajiwa kukamilisha safari ya kutinga robo fainali kwa kukamilisha michezo ya mkondo wa pili hatua ya 16 bora ni Barcelona (Hispani) dhidi ya SSC Napoli (Italia), ambapo katika mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizo zilimaliza kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja. Olympic Lyon (Ufaransa) dhidi ya Juventus (Italia), katika mchezo wa mkondo wa kwanza Lyon walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako