• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: AK yasaidia wanariadha kulipia gharama za karantini

    (GMT+08:00) 2020-05-07 17:05:37

    Shirikisho la RIadha la Kenya (AK) limelipa gharama za karantini na safari ya kurudi Kenya kwa wanariadha wake watano waliowasili nchini humo kutokea India na Malaysia mara baada ya safari za kimataifa kufutwa. Rais wa AK Jackson Tuwei amesema, wanaweza kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kujua wanariadha wangapi wamekwama katika nchi za nje, lakini wanawasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ili kupata msaada. Pia amesema wanawasiliana na balozi za Kenya katika nchi kadhaa ikiwemo India, Malaysia, na China ili kujua idadi kamili ya wanariadha walioko kwenye nchi hizo kutokana na kufungwa kwa mipaka na safari za ndege za kimataifa kutokana na janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako