• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wilaya zote nchini China ziko katika kiwango cha chini cha mlipuko wa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-07 17:23:12

    Msemaji wa Kamati ya Afya ya China Mi Feng amesema, wilaya zote nchini humo ziko katika kiwango cha chini cha hatari ya mlipuko wa virusi vya Corona.

    Pia msemaji huyo ameonya juu ya sintofahamu katika mazingira hayo na kutaka hatua ziendelee kuchukuliwa ili kuzuia mlipuko wa virusi hivyo kutokea tena.

    Hakuna kesi mpya za ndani za maambukizi ya virusi vya Corona katika siku nne mfululizo, na pia hakuna vifo vinavyotokana na virusi hivyo vilivyoripotiwa katika siku 22 zilizopita.

    Wakati huohuo, ripoti iliyotolewa katika Gazeti la Nature la Uingereza imesema, kama China isingedhibiti mlipuko wa virusi vya Corona, zaidi ya watu milioni 7 wangeambukizwa virusi hivyo nchini China mpaka mwishoni mwa mwezi Februari. Ripoti hiyo imesema, hatua ya kugundua na kuwatenga watu walioambukizwa virusi hivyo ilisaidia zaidi kuzuia kuenea kwa maambukizi.

    Ripoti hiyo pia imesema kutosogeleana kwa karibu pia kunaweza kusaidia sana kupunguza maambukizi baada ya marufuku ya kusafiri kuondolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako