• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kushirikiana na WHO katika kutafuta chanzo cha virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-07 18:23:18

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China imeshirikiana na Shirila la Afya Duniani (WHO) kwa wazi juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta chanzo cha virusi vya Corona.

    Hua Chunying amesema hayo leo hapa Beijing, na kuongeza kuwa China inapenda kutoa mchango wake kwa ajili ya kuwahudumia binadamu katika kukabiliana na ugonjwa mkali wa kuambukiza. Amesema kazi ya kutafuta chanzo cha virusi ni ya suala la kisayansi, na inatakiwa kutafitiwa na wanasayansi na wataalamu, ili kupata majibu sahihi kutokana na utafiti wa kutosha. Pia amesisitiza kuwa, jambo linalopingwa vikali na China ni nchi chache husika zinazotaka kuifanya kazi ya kutafuta chanzo cha virusi iwe suala la kisiasa.

    Mkurugenzi wa kiufundi wa Programu za Dharura za WHO Bibi Maria Van Kerkhove jana amesema wamejadili kutuma tena ujumbe tena nchini China, ili kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako