• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapata mkopo wa Sh79.3b (U$739m) kutoka IMF kupambana na Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-07 19:46:59

    Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeidhinisha mkopo wa Sh79.3 bilioni kwa Kenya ili kuisadia nchi hiyo kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

    Huu ni mkopo wa pili kwa Kenya wa kupambana na Corona katika kipindi cha miezi miwili iliyopita tangu maambukizi ya Corona yatangazwe Nairobi.

    Mwezi Aprili,Wizara ya Afya nchini Kenya ilipata Ksh5.3bn kutoka Benki ya Dunia kufadhili uzalishaji wa vitakasa mikono,nguo za kujikinga na maambukizi ya Corona,na kuongeza idadi ya vitanda kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.

    Kwenye taarifa iliyotolewa jana,Bodi ya IMF,ilisema imeidhinisha Kenya kupewa Sh79 bilion (about US$739 million) zitakazotolewa chini ya mpango wa mkopo wa haraka (RCF).

    Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa fedha hizo zitaisadia Kenya kwa kiwango kikubwa katika kupambana na Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako