• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Serikali yaeleza kwa kina kuhusu masuala ya kodi ya umeme

    (GMT+08:00) 2020-05-07 19:47:37

    Wizara ya Nishati nchini Tanzania imelieleza Bunge la nchi hiyo kuwa masuala ya kodi hutozwa na taasisi za kikodi kulingana na sheria za kodi zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.

    Kwa mujibu wa wizara hiyo, masuala ya kikodi hutozwa na taasisi hizo kulingana na sheria na kwamba pamoja na hali hiyo serikali imeendelea kutatua kero mbalimbali za kikodi katika biashara ya umeme kati ya mashirika ya umeme ya Zanzibar (ZECO) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) .

    Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) hununua umeme wa jumla kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), lakini wanaponunua umeme hutozwa kodi ya ongezeko la thamani(VAT) na Mamlaka ya Mapato (TRA) na wanapokwenda kuuza Zanzibar hutozwa tena kodi ya VAT na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) jambo ambalo hupelekea shirika hilo kuwa na madeni makubwa.

    Aidha Wizara hiyo imesema kwa vipindi tofauti TRA na ZRB zimekuwa zikifanya mapitio ya kodi hizo ili kuleta manufaa kwa pande zote mbili za Muungano.

    Pia Wizara hiyo ilieleza kuwa katika hatua ya kupata ufumbuzi wa kudumu katika jambo hilo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) ilifanya marekebisho ya Sheria ya Kodi na Ushuru Mbalimbali ya Mwaka 2019/20 ambapo umeme unaouzwa kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar uliondolewa VAT na kubaki asilimia sifuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako