• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapato ya madereva wa Uber kushuka kutokana na Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-07 19:47:55

    Madereva wa magari ya teksi za Uber wanakabiliwa na kushuka kwa mapato yao kwa kiwango kikubwa baada ya kampuni hiyo kusitisha ukusanyaji wa asilimia 3 ya wanayochukua kwa nauli na kurejesha ada ya asilimia 25 ,ikisema kuwa hiyo imesababishwa na kupungua kwa biashara kutokana na ugonjwa wa Corona.

    Kampuni hiyo imefuta ada ya asilimia 3 inayochukua na kurejesha ile ya zamani ya asilimia 25,ambayo ilipigwa vita na madereva kwa muda mrefu.

    Uber imesema uamuzi huo umetokana na kupungua kwa idadi ya safari kutokana na zuio la kutosafiri lililowekwa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi ikiwa ni pamoja na amri ya kutokuwa nje kuanzia jioni hadi alfajiri pamoja na kufungwa kwa shule,baa na vilabu vya usiku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako