• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Michuano ya Enterprise Cup kufutwa kupisha Ligi Kuu ya Kenya Cup

    (GMT+08:00) 2020-05-08 08:45:15

    Michuano ya Enterprise Cup itafutiliwa mbali katika kalenda ya raga nchini Kenya msimu huu ili kuwezesha vikosi kukamilisha kampeni za Ligi Kuu ya Kenya Cup. Pendekezo hili la wasimamizi wa klabu mbalimbali linatarajiwa kuidhinishwa na Shirikisho la Raga la Kenya (KRU) ambao wamebatilisha maamuzi ya awali ya kufutilia mbali kabisa msimu huu mzima wa raga kutokana na janga la corona. Hadi kusitishwa kwa shughuli zote za michezo chini Kenya mnamo Machi 2020, michuano ya Enterprise Cup ambayo ndiyo ya zamani zaidi katika historia ya raga ya Kenya, yalikuwa yametinga hatua ya nusu-fainali. Mabingwa watetezi Kabras RFC walikuwa wamepangwa kuvaana na Homeboyz huku wanabenki wa KCB wakiratibiwa kumenyana na Impala Saracens. Kwa mujibu wa KRU, itakuwa busara kufutilia mbali kipute cha Enterprise Cup ili kupunguza mrundikano wa mechi katika kalenda ya msimu huu pindi michuano ya raga ya Kenya Cup itakaporejea baada ya corona kudhibitiwa vilivyo. Kwa mujibu wa Xavier Makuba ambaye ni mwenyekiti wa michuano ya Kenya Cup, kinyang'anyiro hicho kimepangwa kurejea Julai 2020 na maamuzi hayo yamechochewa na ukubwa wa kiwango cha fedha zilizowekezwa kwa minajili ya mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako