• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ander Herrera asema hakutaka kuondoka Man UTD

    (GMT+08:00) 2020-05-08 16:56:04

    Aliyekua kiungo wa Mashetani Wekundi (Manchester United) Ander Herrera, amefichua siri ya safari ya kuondoka klabuni hapo, kwa kusema hakupenda iwe hivyo kama ilivyochukuliwa na mashabiki wengi duniani. Herrera ambaye kwa sasa anakipiga na mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, amesema alitamani kuendelea kuitumikia Manchester United lakini mamwazo yake hayakuwa sawa na bodi ya uongozi ya Manchester United. Amesema siku zote aliamini angedumu kwa mda mrefu klabuni hapo kutokana na mapenze ya dhati aliyokua nayo, lakini cha kushangaza aliingizwa kwenye orodha ya wachezaji waliouzwa mwishoni mwa msimu uliopita. Julai 04 – 2019, Herrera alisaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Paris Saint-Germain, akiwa kama mchezaji huru, na Septemba 14 alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa Ufaransa dhidi ya Strasbourg waliokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri, akichukua nafasi ya Pablo Sarabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako