• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Eymael achekelea ligi kurejea

    (GMT+08:00) 2020-05-08 17:03:07

    Kocha Mkuu wa Young Africans, Mholanzi Luc Eymael amefurahishwa na taarifa za matarajio ya kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ilisimama mwezi Machi kupisha vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona. Kocha huyo ambaye kwa sasa yupo nchini kwao Uholanzi, amesema taarifa za matarajio ya kurudi kwa ligi hiyo amezipokea kwa mikono miwili na alikua anatamani iwe hivyo, kutokana na kuamini bado kikosi chake kinahitaji kupambana hadi mwisho wa msimu. Awali kocha Luc aliwahi kupendekeza wachezaji wa kila timu wapimwe na kuweka karantini, na wasiruhusiwe kwenda popote, ili kufanikisha mpango wa kuchezwa kwa kwa ligi kuu. Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa alama zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa alama zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na alama 50 za mechi 28. Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa alama zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC alama 22 mechi 28, Alliance FC alama 29, mechi 29, Mbeya City alama 30 mechi 29 na Ndanda FC alama 31 mechi 29.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako