• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua ya wazi iliyoandikwa na muuguzi aliyetoa msaada kwa mkoa wa Hubei kwa rais Donald Trump wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-05-08 18:44:11

    Mheshimiwa rais Trump:

    Shikamoo. Mimi ni muuguzi wa kitengo cha upumuaji, ambaye nimerudi baada ya kutoa msaada kwa hospitali ya mji wa Wuhan. Nilishirikiana na wenzangu elfu 42 kutoa msaada mkoani Hubei pamoja na wahudumu wa afya wa mkoa huo. Nakuandikia barua ili kukuelezea mambo yaliyotokea mjini humo.

    Nilifunga safari katika mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina, ambao ni kama mkesha wa Krismasi nchini Marekani. Katika siku hiyo ambayo ni muhimu kwa familia za wachina kukutana, nilifahamu ni jukumu langu kuokoa maisha ya watu. Tukiwa na wazo kama hilo, mimi na wenzangu elfu 42 tuliagana na jamaa zetu kwenda mjini Wuhan kuanza mapambano dhidi ya virusi.

    Mwanzoni, tulikumbwa na tatizo la ukosefu wa vifaa vya matibabu. Ili kubana matumizi ya vifaa hivyo, tulikuwa hatutaki kuvua nguo za kujikinga hata tulipolowa jasho mwili wote na kushindwa kupumua. Ndiyo maana naweza kuelewa hisia za baadhi ya madaktari wa Marekani waliochukua mifuko ya plastiki na kuvaa kama nguo ya kujikinga. Na pia naona uchungu nilipoona jamaa za madaktari wa Marekani wakichukua picha zao huku wakitokwa machozi kwa masikitiko.

    Sasa siku zenye shida kubwa zimepita. Jambo linalonifurahisha ni kuona wagonjwa wengi wamepona na kuondoka hospitali, haswa wale wenye umri mkubwa. Tunamtendea kila mzee kama tunavyowatendea wazazi wetu wenyewe, na wazee zaidi ya 3,600 wenye umri wa miaka zaidi ya 80 wamepona. Naona furaha tena fahari kubwa, kwani wazee hao waliwahi kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya maisha yetu ya sasa, na nimepata fursa ya kuokoa maisha yao kadiri niwezavyo.

    Mjini Wuhan, tulijitahidi tunavyoweza kuokoa watu wote, bila ya kujali ni mzee mwenye umri wa miaka 108, au mtoto aliyezaliwa saa 30 zilizopita. Ni jukumu letu kuwaokoa, kwani maisha ni muhimu kuliko kitu kingine chochote.

    Mheshimiwa rais, hizi ni simulizi za yaliyotokea mjini Wuhan.

    Najua wakati huu Wamarekani wengi wanavumilia adha kubwa inayotokana na maambukizi ya virusi, na wahudumu wengi wa afya wa Marekani wanapambana kwenye mstari wa mbele, vilevile kuna watu wengi wa kawaida wanaowatunza wengine kwa njia tofauti. Nataka kutoa heshima kwao! Pia nawatakia kila la heri wamarekani kwa moyo wangu wa dhati!

    Muuguzi mmoja aliyetoa msaada mkoani Hubei

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako