• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha anga cha China kinachobeba binadamu charudi sayari ya dunia kwa mafanikio

    (GMT+08:00) 2020-05-08 18:54:39

    Mamlaka ya Safari za Anga ya Juu ya China CMSA imesema, chombo cha anga cha kizazi kipya cha China kinachobeba binadamu kilichorushwa kwa majaribio katika anga ya juu kimerudi leo katika mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China.

    Mamlaka hiyo imesema, majaribio hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa. chombo hicho kimesafiri kwenye njia ya usafiri wa anga kwa siku mbili na saa 19, kimetua leo kwenye sayari ya dunia saa saba na dakika 49 mchana kwa saa za China, na kimefanya majaribio mfululizo ya kisayansi na ya kiteknolojia juu ya mambo ya anga ya juu.

    Mamlaka hiyo imeongeza kuwa chombo hicho cha kizazi kipya ni chombo cha anga ya juu cha kisasa kinachoweza kufanya opresheni za aina mbalimbali, ikiwemo kazi ya uchunguzi wa sayari ya Mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako