• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko la matumizi la China lafufuka kwa kasi zaidi kwenye kipindi cha likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani

    (GMT+08:00) 2020-05-08 18:55:05

    Wizara ya Biashara ya China leo imesema kutokana na matokeo mazuri ya udhibiti wa kuenea kwa virusi vya Corona nchini China, soko la matumizi nchini humo limefufuka kwa kasi zaidi kwenye kipindi cha likizo ya siku 5 ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

    Naibu waziri wa wizara hiyo Bw. Wang Bingnan amesema, janga la virusi vya Corona limeongeza kasi ya matumizi kwenye mtandao wa internet, sekta ambayo imeongezeka kwa asilimia 36.3 kwenye kipindi hicho ikilinganishwa na mwaka jana. Mbali na hayo, uuzaji wa magari na mashine za nyumbani pia umeongezeka, na kwamba kuuza bidhaa kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni imekuwa njia mpya inayopendwa na makampuni mengi.

    Wakati huohuo, sekta ya utalii nchini China pia imefufuka kwa kasi kwenye kipindi hicho cha mapumziko, ambapo China ilipokea watalii wa ndani milioni 115, na kupata dola takriban bilioni 6.72 za kimarekani kwenye sekta ya utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako