• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima ndizi mkoani Mbeya walilia kudorora kwa soko

    (GMT+08:00) 2020-05-08 20:20:41

    Wakulima wa zao la ndizi mkoani Mbeya, wamelalamikia ukosefu wa soko la uhakika baada ya wateja wao kutoka nje ya nchi ikiwamo Afrika Kusini, Malawi na Congo kutoingia nchini humo kkwa kuhofia maambukizo ya virusi vya corona.

    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe mkoani Mbeya, Ezekiel Mwakota, amesema kuwa kwa sasa hali ya soko la ndizi sio ya kuridhisha kutokana na zao hilo kukosa kabisa wateja.

    Amesema wateja wengi hawawezi kufika nchini humo kufuatia kufungwa kwa mipaka kutokana na ugonjwa wa Covid-19 ambao umesambaa nchi mbalimbali. Alisema zao la ndizi katika eneo la Rungwe linachangia kwa kiasi kikubwa pato la halmashauri, hivyo kudorora kwake kutasababisha mapato kushuka na kukwamisha shughuli nyingine za maendeleo ambazo zinategemea ushuru wa zao hilo.

    Alisema asilimia 90 ya wakazi wa wilaya hiyo inategemea kilimo cha ndizi kuendesha maisha yao hivyo kudorora kwa soko kunaumiza makundi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako