• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara watakiwa kuchangamkia fursa ya madini

    (GMT+08:00) 2020-05-08 20:22:37

    Wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya ununuaji wa madini kutoka kwa wachimbaji, baada ya serikali kulegeza masharti kutokana na janga la ugonjwa wa corona. Akizungumzia athari ya virusi vya Corona kwenye sekta ya madini, rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (Femata), John Bina, amesema serikali imeruhusu mtu yeyote mwenye mtaji wa kununua madini afuate taratibu zilizowekwa, na imeondoa baadhi ya vizuizi kwa wanunuzi kununua kwenye masoko ya madini. Bina amesema ugonjwa huo umeathiri soko kwa kuwa madini mengi huuzwa nje ya nchi.

    Aliwashawishi wanunuzi wenye uwezo mkubwa kifedha kuendelea kununua madini kwa kufuata taratibu zilizowekwa na serikali.Aidha Aliwataka wachimbaji kufuata masharti na maelekezo yanayotolewa na serikali namna ya kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako