• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imeshalipa ada zote za uanachama katika Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-05-08 21:17:29

    Msemaji wa mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema China inatekeleza kwa makini majukumu yake ya kifedha kwa Umoja wa Mataifa, na imelipa ada zote za uanachama katika Umoja huo kwa mwaka huu, ili kuunga mkono kihalisi kazi za Umoja wa Mataifa.

    Amesema kulipa ada zote kwa wakati ni jukumu linalopaswa kutekelezwa na nchi wanachama wa Umoja huo, hasa kwa nchi kubwa ambazo zinatakiwa ziwe mfano kwa nchi nyingine, ili kusaidia Umoja wa Mataifa kukabiliana na hali ngumu ya kifedha kwa sasa.

    Ameongeza kuwa, hivi sasa jumuiya ya kimataifa inakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo virusi vya Corona, hivyo nchi zote zinatakiwa kushikilia utaratibu wa pande nyingi na kulinda mfumo wa kimataifa wenye kiini cha Umoja wa Mataifa. Amesema China inapenda kushirikiana na pande zote kufanya kazi kubwa zaidi katika kuhimiza amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako