• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ajibu ujumbe kutoka kwa mwenzake wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2020-05-09 19:56:11

    Rais Xi Jinping wa China ametoa ujumbe wa kumshukuru mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na kusema, anafurahi kupata ujumbe wa kirafiki kutoka kwa rais Kim Jong Un. Mwezi Februari Bw. Kim Jong Un, alitoa salamu kwa China, juu ya mlipuko wa virusi vya Corona na kueleza uungaji mkono wake kwa China, ambao umeonesha urafiki wa dhati kati ya serikali na watu wa nchi hizo mbili.

    Rais Xi amesema, chini ya uongozi wa serikali kuu ya China na uungaji mkono kutoka sekta mbalimbali, kazi ya kupambana na mlipuko huo hapa China imepata mafanikio makubwa. Amesema anafuatilia hali ya mapambano hayo nchini Korea Kaskazini na hali ya afya ya watu wa nchi hiyo. Anafurahia hatua zilizochukuliwa chini ya uongozi wa rais Kim Jong Un za kupambana na virusi hivyo na kutaka zipate mafanikio.

    Rais Xi pia amesema China inapenda kuongeza ushirikiano wa kupambana na virusi hivyo na Korea Kaskazini na kutoa misaada kadiri iwezavyo kulingana na mahitaji ya Korea Kaskazini. Ana imani kuwa, chini ya jitihada za nchi hizo mbili, mapambano dhidi ya virusi vya Corona yatashinda.

    Habari zinasema, juzi, rais Kim Jong Un alitoa ujumbe kwa rais Xi Jinping na kusifu mafanikio yaliyopatikana na China katika kupambana na virusi hivyo. Amemtakia rais Xi awe salama na kutarajia uhusiano kati ya vyama vya nchi hizo mbili uendelee zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako