• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Eliud Kipchoge apambana na COVID-19 kwa kuwapa wenzake chakula

    (GMT+08:00) 2020-05-11 15:49:17

    Eliud Kipchoge amejiunga na Wakenya wengine katika vita dhidi ya virusi vya corona kwa kutoa msaada wa chakula kwa wanariadha wasiojiweza. Kipchoge amekuwa akisafiri katika kaunti tofauti eneo la Bonde la Ufa kusaidia katika kutoa vyakula hivyo kwa wenzake ambao wameathiriwa pakubwa na janga hilo. Jumamosi, Mei 10, wanariadha 59 kutoka eneo la Bonde la Ufa Kaskazini walipokea msaada wa chakula kuwalinda wakati huu mgumu, huku Kipchoge akiongoza zoezi hilo. Bingwa huyo mwenye miaka 35, aliteuliwa hii majuzi kuwa balozi wa mradi huo uliozinduliwa na Wizara ya Michezo. Bingwa huyo mshikilizi wa mbio za London Marathon amekabithiwa jukumu hilo la kuwafikia wanariadha ambao wamepata pigo kufuatia kufutwa kwa shughuli za michezo. Chakula hicho kilitolewa na Wizara ya michezo pamoja na wakfu wa Eliud Kipchoge na wasamaria wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako