• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Beki Mkenya awataka Simba watulie, anakuja

    (GMT+08:00) 2020-05-11 15:51:09

    Beki wa kati Mike Kibwage ambaye ni raia wa Kenya ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Simba kuwa atakuja kuichezea timu yao kama watampa ofa nzuri. Simba iko kwenye mkakati wa kuhakikisha inasuka safu yake ya ulinzi ambayo Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck anaonekana kutoridhishwa nayo kwa madai inaruhusu sana mabao. Inaaminika Kocha huyo anafuatilia mabeki wengi baadhi yao ni Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union, Yakubu Mohammed anayekipiga Azam FC na sasa Kibwage anayecheza KCB ya Kenya inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo ameongezeka. Kibwage ameweka wazi kuwa licha ya kuwa hajafuatwa rasmi ya Simba lakini yuko tayari kutua kikosini humo na kufanya makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako