• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Sarpong asema akitua Yanga, Simba SC watakiona

    (GMT+08:00) 2020-05-11 15:51:36

    Mshambuliaji wa Rayon Sport ya Rwanda, Mghana, Michael Sarpong amefichukua kuwa amekuwa akiisikia ugumu Ligi Kuu Bara lakini haiwezi kumpa hofu kwani amepanga akitua tu Yanga basi atazifunga timu zote atakazokutana nazo ikiwemo Simba. Mshambuliaji huyo kwa sasa amekuwa ni mchezaji huru baada ya Rayon kuvunja mkataba wake kutokana na madai ya utovu wa nidhamu licha ya msimu uliopita kufanikiwa kufunga mabao 16 yaliyosaidia kuipa ubingwa wa Rwanda. Tayari Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Mhandi Hersi Said na mwenyekiti wa timu hiyo, Dk Mshindo Msolla wamezungumza na wakala wa mshambuliaji huyo kwa ajili ya kujiunga na Yanga kutokana na mapendekezo ya kocha wa Yanga, Luc Eymael. Sarpong alisema kuwa licha kuwa wana ofa nyingi lakini kama atafanikiwa kujiunga na Yanga basi amepanga kuona anafunga katika kila mchezo atakaocheza kwa lengo la kuisaidia timu yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako