• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mlandege watakiwa kuepuka mikusanyiko

    (GMT+08:00) 2020-05-11 15:52:13

    Rais wa timu ya Mlandege ya Zanzibar, Mbaraka Hamid, amewataka wachezaji wake na wa timu nyingine kuendelea kufuata maelekezo ya serikali katika kipindi hiki cha kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona. Hamid amesema ni vizuri katika kipindi hiki wachezaji wakafanya mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka sawa ili kuepuka mikusanyiko kama ilivyoelekezwa na serikali. Mpaka wakati Ligi zinasimamisha ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, timu ya Mlandege inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar ilikuwa nafasi ya nne na point 44, huku KMKM ikiongoza Ligi hiyo kwa alama 46.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako