• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu kwa wauguzi kote nchini wakati wa Siku ya KImataifa ya Wauguzi na Wakunga

    (GMT+08:00) 2020-05-11 17:25:01

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za dhati kwa wauguzi kote nchini humo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wauguzi na Wakunga.

    Rais Xi ameeleza kuwa, baada ya kutokea kwa janga la maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19), idadi kubwa ya wauguzi walipambana kwenye mstari wa mbele, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi na kulinda usalama na afya ya watu wa nchi mbalimbali, wakionesha moyo wao unaoshikilia maadili.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, kazi ya uuguzi inachukua sehemu muhimu katika mambo ya afya. Anatumai wauguzi wataendeleza mila nzuri na kuonesha moyo wa kibinadamu, ili kuchangia katika ujenzi wa afya nchini China na kulinda usalama wa afya ya umma duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako