• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kumbukumbu za kukua kwa Rais Xi na mama yake

    (GMT+08:00) 2020-05-11 17:25:41

    "Mama anashona nguo kwa ajili ya mtoto wake atakayefunga safari ndefu. Mtoto akichukua moyo wa dhati anataka kutoa shukurani kwa mama yake." Rais Xi Jinping wa China alisoma shairi hili hodari la Enzi ya Tang wakati wa mwaka mpya wa jadi wa kichina wa mwaka 2015.

    Kwa rais Xi Jinping, "Familia ni darasa la kwanza kwa watu, na wazazi ndio walimu wa kwanza." Hayo ndio maneno aliyokuwa anaambiwa na mama yake Bibi Qi Xin, na anayakumbuka maneno hayo hadi leo.

    Katika maadhimisho ya siku ya Mama ya mwaka huu, Televisheni ya taifa ya China CCTV imetoa maelezo kuhusu kumbukumbu za utoto wa rais Xi Jinping, na mafunzo aliyopata kutoka kwa mama yake yalivyomfaa katika maisha yake.

    Mama wa rais Xi aliwahi kusema "Wazazi na watu wazima wanatakiwa kurithisha maadili mazuri kwa watoto wao wakiwa bado wadogo, kuwasaidia kujenga maadili ya kuwa waadilifu na watu wema, ili wakue na kuwa watu watakaotoa mchango kwa nchi na umma kwa ujumla.

    Maadili ya familia ya Xi ni kuwafundisha watoto kwa nidhamu makini, na kutofanya matumizi ya hovyo. Mama yake rais Xi amekuwa akitoa mfano mzuri wa tabia hiyo wakati wa kuwalea watoto, na kufanya kazi kwa bidii bila ya kujali matatizo gani makubwa yanamkabili, na rais Xi amerithi vizuri maadili hayo.

    Kwa kweli ni furaha kubwa kwa mama ikiwa mtoto wake akiwa salama na mwenye furaha. Kwa mama yake rais Xi, ana matumaini makubwa zaidi kuwa Xi Jinping atawajibika kwa nchi na watu wa China. Wakati rais Xi alipokuwa na umri wa miaka mitano hadi sita, mama yake alimsimulia hadithi kuhusu shujaa wa enzi ya Nan Song ya China Yue Fei ambaye alipambana na maadui wa taifa kwa ushujaa. Kuanzia hapo, rais Xi anakumbuka kuwa anapaswa "kuitumikia nchi kwa utiifu mkubwa."

    Wakati wa mwaka mpya wa jadi wa kichina wa mwaka 2001, rais Xi alishindwa kurudi Beijing kukutana na wazazi wake kutokana na sababu ya kazi, alipoambiwa hivyo, mama yake aliona fahari, "Juhudi zako zinaonesha vizuri moyo wako wa kututunza, hii inaonesha uwajibikiaji wako kwa familia na pia kwako wewe mwenyewe."

    Katika ofisi ya rais Xi, kuna picha nyingi za rais Xi akiwa na wazazi wake, moja ni yeye akitembea kwenye bustani pamoja na mama yake. Rais Xi anamtunza vizuri mama yake. Baadhi ya wakati baada ya kula chakula, rais Xi anaambatana na mama yake kutembelea nje na kuongea naye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako