• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapeleka wataalam wa afya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchini Zimbabwe, DRC na Algeria

    (GMT+08:00) 2020-05-11 19:24:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Zhao Lijian amesema, serikali ya China imepeleka timu ya wataalam wa afya katika nchi za Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) na Algeria, ili kuzisaidia kukabiliana janga la virusi vya Corona.

    Bw. Zhao amesema, timu hiyo imeanzishwa na Tume ya afya ya kitaifa, na inaundwa na wataalamu kutoka tume ya afya ya mkoa wa Hunan, Hebei na mji wa Chongqing. Timu inayoelekea nchini Zimbabwe imeondoka leo, na timu nyingine zinazoenda nchini DRC na Algeria zitaondoka hivi karibuni.

    Bw. Zhao ameongeza kuwa, China itaendelea kutoa vifaa zaidi vya kupambana na janga hilo kwa nchi za Afrika kadri hali inavyoendelea barani humo na kwa mahitaji ya nchi za Afrika. Amesema China inafanya hivyo ili kuimarisha ushirikiano kati yake na Afrika katika sekta ya afya ya umma, kuzuia na kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo, na kufanya kazi kwa pamoja ili kupata ushindi wa mwisho wa janga hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako