• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Soka ya Uingereza bado ni kizungumkuti

    (GMT+08:00) 2020-05-12 08:34:37

    Chama cha soka ulaya (UEFA) kimeripotiwa kuwa kitaongeza muda mbele zaidi endapo Ligi Kuu England hawatokuwa wamefikia muafaka wa namna ya kurejesha Ligi hadi ifikiapo Mei 25 2020. Rais wa UEFA Aleksander Ceferin amethibitisha hilo baada ya mwezi uliopita kutoa maagizo hayo ili kuhakikisha kuwa klabu na viongozi wa EPL wanakuja na mpango wa namna ya kumalizia msimu 2019/20. Katika hatua nyingine serikali ya Uingereza imetangaza kuwa hakuna michezo itakayoruhusiwa kuendelea kipindi hiki hata kama ni bila mashabiki. Taarifa ya serikali imeeleza kuwa zuio hilo ni hadi Juni 1, 2020 ambapo utatangazwa muelekeo mpya kutokana na mwenendo wa janga la Corona utakavyokuwa. Wakati huohuo klabu za Ligi Kuu Uingereza zinatarajiwa kurejesha jumla ya Sh bilioni 47 kwa kampuni za upeperushaji mechi zao za kitaifa na kimataifa hata kama michuano tisa iliyosalia msimu huu itasakatwa ndani ya viwanja vitupu bila mashabiki. Vikosi vyote 20 vya EPL vilionywa kwamba huenda kiasi hicho cha fedha kikaongezeka zaidi iwapo msimu huu mzima utafutiliwa mbali au pasiwepo kikosi chochote kitakachoshushwa ngazi katika kampeni za muhula huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako