• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wolfsburg yapata pigo baada ya nyota wake kujeruhiwa usoni

    (GMT+08:00) 2020-05-12 08:35:00

    Kiungo wa Wolfsburg Yannick Gerhardt amepata jeraha baya usoni baada ya kugongana kichwa na mchezaji mwenzake na kupasuka wakati wa mazoezi. Ajali hiyo ilitokea wakati wa mechi ya mazoezi ya vikosi viwili vya wachezaji 11 kwa 11. Kocha Oliver Glasner alisena katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya video kwamba kujeruhiwa kwa Gerhardt ni pigo kubwa kwa klabu hiyo wakati huu timu hiyo ikijiandaa kujiimarisha na Bundesliga itakayoanza kutimua vumbi tena Mei 16. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amelazwa hospitali na lazima afanyiwe upasuaji. Madaktari wa vilabu vya Ujerumani walionya awali kwamba huenda kukatokea ongezeko la majeraha kufuatia miezi miwili ya ligi kusimama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako