• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Besiktas yafunga mtambo kiwanjani ili kunusuru wachezaji na corona

    (GMT+08:00) 2020-05-12 08:35:49

    Miamba ya soka Uturuki, Besiktas wameweka mtambo maalumu wa vipimo kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo baada ya mchezaji mmoja na mfanyakazi kubainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19. Wachezaji wa Besiktas kabla ya kuanza mazoezi watalazimika kupita katika mtambo huo maalum uitwao 'enormous disinfection cabinet' na kuingia uwanjani. Klabu mbalimbali nchini Uturuki zimeanza mazoezi ya kuendelea na msimu ambao unatarajiwa kurejea mwezi Juni, Ligi Kuu Uturuki ilisitishwa Machi 19 kutokana na janga la virusi vya corona linalotikisa dunia. Mtambo huo wenye unyevu una pande 20, wachezaji na wafanyakazi watalazimika kuingia huku kila mmoja akiwa amevaa barakoa kabla ya kushiriki mazoezi kama moja ya hatua za kupunguza maambukizi ya virusi vya corona. Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo, Nihat Ozdemir alitangaza kwenye mkutano wa video siku nne zilizopita kuwa michezo itaanza tena mwezi ujao katika viwanja vitupu kwa lengo la kukamilisha msimu husika ifikapo Julai 26. Upande wake Waziri wa Afya nchini humo, Fahrettin Koca alipinga maamuzi hayo akisema Shirikisho lilichukua uamuzi huo kwa hiari yake, kwa hivyo, jukumu linaangukia kwenye shirikisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako