• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza upandaji wa mayungiyungi kwenye kupambana na umaskini

    (GMT+08:00) 2020-05-12 14:45:06

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza upandaji mayungiyungi wa kila siku ili kuwasaidia wenyeji kupambana na umaskini.

    Rais Xi amesema alisema hayo jana mchana alipotembelea shamba la maua ya yunguyungi katika mji wa Datong, baada ya ziara ya ukaguzi mkoani Shanxi.

    Alipotembelea shamba hilo Rais Xi aliongea kwa karibu na wanakijiji wanaofanya kazi katika shamba hilo. Rais Xi alifurahi kujua kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uongozi wa mashirika makubwa na vyama vya ushirika, shamba hilo limekuwa na uzalishaji uliotulia na wenye ubora na kuwa na uhakika wa soko na bei, na kuzisaidia kaya za eneo hilo kutoka kwenye umaskini.

    Rais Xi amesema maua hayo yanaweza kuendelea na kuwa sekta kubwa yenye matarajio. Amesisitiza kufanyika juhudi za kuendeleza kilimo cha maua hayo na kukifanya kitoe mchango kamili kwenye kupunguza umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako