• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Niyonzima ahamia ufukweni

    (GMT+08:00) 2020-05-12 15:44:41

    Kiungo wa Young Africans Haruna Niyonzima amesema wakati huu Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imesimama, anaendelea kujiweka sawa tayari kwa kuisaidia timu yake pale ligi itakaporejea. Pamoja na kutekeleza program ya mazoezi ya timu, nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda amesema kila siku jioni hufanya mazoezi ufukweni akijumuika na wachezaji wa timu mbalimbali. Niyonzima amekuwa na mwanzo mzuri katika awamu yake ya pili kunako klabu ya Young Africans aliyojiunga nayo mwezi Januari 2020. Kwa mara ya kwanza Niyonzima alisajiliwa na Young Africans mwaka 2012, akacheza kwa misimu mitano kisha kujiunga na Simba mwaka 2017 ambako alicheza kwa misimu miwili. Alirejea Young Africans akitokea klabu ya AS Kigali ya kwao Rwanda ambayo aliitumikia kwa miezi sita tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako