• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kiungo wa Simba asema yuko tayari kujiunga na Yanga SC kama wakimuhitaji

    (GMT+08:00) 2020-05-12 15:49:05

    Kiungo mchezeshaji fundi wa Simba, Mohammed Ibrahim amesema kuwa yupo tayari kujiunga na Yanga kwenye msimu ujao kama wakihitaji saini yake. Nyota huyo anayekipiga kwa mkopo Namungo FC ya Lindi, ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Mastaa wengine wanaomaliza mikataba yao Simba ni Yusuph Mlipili, Pascal Wawa, Sharraf Shiboub, Deo Kanda na Hassani Dilunga wanaotarajiwa kuongezewa mikataba. Mo amesema tayari baadhi ya klabu zimemfuata na kumpa ofa ambazo zipo kwenye majadiiliano ya dau la usajili ambalo yeye analitaka ili asaini. Amesema kati ya timu ambazo zimempa ofa ni Namungo anayoichezea kwa ajili ya kumpa mkataba mrefu wa kubaki kuendelea kukipiga hapo, licha ya yeye kuwa na mpango wa kuondoka hapo. Aliongeza kuwa ni wakati muafaka wa yeye kutoka hapo na kwenda kutafuta changamoto nyingine mpya kwenye moja ya klabu ili kurejesha heshima yake iliyopotea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako