• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza kuondoa ushuru wa ziada kwa bidhaa zaidi kutoka Marekani

    (GMT+08:00) 2020-05-12 16:47:10

    Chine leo imetoa orodha mpya ya bidhaa zitakazoondolewa ushuru wa ziada katika raundi ya pili ya bidhaa zinazotoka nchini Marekani.

    Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Ushuru wa Forodha iliyo chini ya Baraza la Serikali la China imesema, hii ni orodha ya pili ya bidhaa kutoka Marekani zinazoondolewa kutoka raundi ya pili ya kujibu hatua ya kifungu cha 301 cha Marekani, na itatumika kuanzia tarehe 19 mwezi huu hadi tarehe 18, Mei, 2021. Pia taarifa hiyo imesema, ushuru ambao tayari ulilipwa utarejeshwa.

    Taarifa hiyo imesema, kwa bidhaa za Marekani ambazo haziko kwenye orodha ya kwanza na ya pili, kamati hiyo imeshauri viwanda kuomba kuondolewa ushuru wa ziada kufuatia orodha ya bidhaa maalum kwa kampuni za ndani zinazopanga kufikia makubaliano na kusafirisha bidhaa hizo kutoka nchini Marekani katika mfumo wa soko la kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako