• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China kushiriki kwenye mkutano wa video wa mawaziri wa mambo ya nje wa SCO

    (GMT+08:00) 2020-05-12 18:29:49

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi kesho hapa Beijing atashiriki kwenye Mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO utakaofanyika kwa njia ya video.

    Bw. Zhao Lijian ameeleza kuwa, katika mkutano huo, mawaziri hao watajadiliana kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, hali ya kimataifa na ya kikanda, na maendeleo ya jumuiya hiyo katika kipindi kijacho.

    Bw. Zhao anaamini kuwa, pande zote zinazohusika zitaimarisha ushirikiano na kuhimiza jumuiya hiyo kutoa mchango kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo na kulinda usalama na maendeleo ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako