• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe inashitisha uagizaji wa nguo za mtumba kuzuia kuenea kwa virusi vya corona

    (GMT+08:00) 2020-05-12 20:46:58
    Wafanyabiashara wa mpaka, ambao wanatengeneza pesa kutokana na kununua na kuuza bidhaa kutoka kwa nchi jirani,wanakaidi kanuni za kufungwa kwa nchi kwa kuvunja sheria na kwenda nchi kama Afrika Kusini na Msumbiji, kulingana na mamlaka.

    Monica Mutsvangwa, Waziri wa Habari, amesema shughuli za ujasusi hususan katika mpaka mkubwa wa Msumbiji ni tishio kubwa kwani kesi za korona zinazoingizwa zinaongezeka.

    Zimbabwe ilipiga marufuku uagizaji wa nguo za mtumba mnamo mwaka wa 2015 kulinda tasnia ya nguo nchini, lakini ililegeza kamba miaka miwili baadaye kwani ndio chanzo kikubwa cha mapato kwa wafanyabiashara wasio rasmi waliomia sana kushuka kwa uchumi.

    Wafanyabiashara wanatoa nguo kutoka Tanzania, Msumbiji, Afrika Kusini na Zambia kuuza kwa wenyeji ambao mapato yao ni ya chini, kuweza kununua nguo mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako