• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Mkenya Wanjiru Karani ateuliwa katika Tume ya Wanawake ya CAT

    (GMT+08:00) 2020-05-13 08:27:33

    Mkenya Wanjiru Mbugua Karani ameteuliwa katika Tume ya Wanawake ya Chama cha Tenisi barani Afrika (CAT), ambayo makao yake ni nchini Tunisia. Wanjiru, 45, ni Mkenya wa kwanza kutumikia tume hiyo ya watu saba. Tume hiyo inaongozwa na Mtunisia Salma Mouelhi-Guizani ambaye ni Rais nao Wanjiru kutoka Kenya, Sallah Adjoa (Togo), Rashika Aboushousha (Misri), Aida Baira (Algeria), Philippina Frimpong (Ghana) na Fatime Kante (Ushelisheli) ni wanachama. Wanjiru ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Tenisi Kenya kwa kipindi cha miaka mitano sasa amesema wameteuliwa kutumikia kwa kipindi cha mwaka 2020 na 2021, na kwamba ni heshima kubwa kupata kuwatumikia wanatenisi wanawake kupitia cheo hicho kipya. Wanjiru aliiwakilisha Kenya kimataifa katika michezo ya chipukizi na pia watu wazima kabla ya kustaafu na kuingia ukocha na usimamizi wa tenisi. Pia ni Mkenya wa kwanza kuhudumu katika Kamati ya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF) inayoshughulikia masuala ya usawa wa jinsia. Aliteuliwa kuhudumu ITF Disemba 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako