• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Memphis Depay kusepa Olympique Lyon kisa kukosa Uefa

    (GMT+08:00) 2020-05-13 08:29:20

    Nyota wa Kidachi, Memphis Depay ameripotiwa anaweza kuhama Olympique Lyon baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya kutokana na msimu wa Ligue 1 kusitishwa. Depay, aliyewahi kuichezea Manchester United amekuwa sehemu ya kikosi cha Lyon ambacho kimeshindwa kujikatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23. Lyon wanaoshika nafasi ya saba walikuwa wakipambana kusaka tiketi ya kucheza Ulaya, lakini bada ya ligi kusitishwa jambo hilo limeshindikana na sasa wametishia kwenda mahakamani. Mmiliki wa klabu hiyo, Jean-Michel Aulas ameibua wasiwasi wake huenda wakapoteza wachezaji wao nyota akiwamo Depay kama hawatawapa nafasi ya kucheza soka ya Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako