• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya Airways yaomba ruzuku  ya dharura ya shilingi bilioni 7

    (GMT+08:00) 2020-05-13 20:37:22
    Shirika la ndege la Kenya Kenya Airways limeomba serikali ruzuku ya dharura ya shilingi bilioni 7 baada ya kusimamisha oparesheni kutokana na janga la corona.

    Wizara ya fedha inakagua maombi hayo ambayo yatawezesha shirika hilo kutengeneza ndege zilizoharibika, malipo ya mishahara ya wafanyikazi na malipo ya bili za matumizi kama usalama, maji, umeme na ada ya maegesho.

    Ndege kubwa hulipa ada ya ya maegesho ya dola 25 kila siku kuegesha katika viwanja vya ndege kama Jomo Kenyatta dola 585 kutua mchana na dola 702 kutua usiku.

    Mbali na ruzuku hiyo shirika hilo pia linaomba misaada mingine kama msamaha wa ushuru na ada za kutua na maegesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako