• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mauzo ya chai Rwanda yaongeka

    (GMT+08:00) 2020-05-13 20:37:44
    Takwimu za Bodi ya Kitaifa ya Maendeleo ya Uuzaji nje wa bidhaa za Kilimo nchini Rwanda (NAEB) imesema nchi hiyo iliuza zaidi ya tani 9 za chai iliyosindikwa yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 27.6 kati ya Januari na Machi 2020.

    Utendaji huo unawakilisha kuongezeka kwa idadi ya mapato ya asilimia 15 na uzalishaji wa asilimia 27 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019.

    Afisa wa mawasiliano wa NAEB Pie Ntwari amesema upanuzi wa mashamba ya chai, uboreshaji wa bei katika soko la kimataifa ni baadhi ya sababu zilizosababisha kukua kwa mauzo ya bidhaa hiyo.

    Alisema biashara ya uuzaji nje wa chai haikuathiriwa vibaya na janga la COVID-19 kipindi hicho na kwamba mzunguko wa chakula bado unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako