• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Nicolas Wadada wa Azam FC awasamehe wapangaji wake kodi

    (GMT+08:00) 2020-05-14 08:32:07

    Beki chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Azam FC Nicolas Wadada amewasamehe wapangaji wake kodi kutokana na kupitia wakati mgumu wa kupambana na janga la Virusi vya Corona. Wadada ambaye ni raia wa Uganda amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na agizo la Serikali ambayo imewaomba wamiliki kufanya hivyo. Taarifa iliyotolewa Kwenye Ukurasa rasmi wa Instagram wa Azam imeeleza kuwa beki huyo ameamua kuwasamehe kodi wapangaji wake. Mwenyewe amesema ana nyumba ambayo aliwapangisha wapangaji na ilikuwa inaniingizia kipato ila kutokana na agizo la Serikali kutaka kuwasamehe kodi wapangaji kutokana na janga la Virusi vya Corona naye amefanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako