• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Serie A kurejelewa rasmi Juni 13

    (GMT+08:00) 2020-05-14 16:49:51

    Kipute cha Ligi Kuu ya Italia (Serie A) sasa kitarejelewa Juni 13, 2020 iwapo serikali itaidhinisha maamuzi ya vinara wa soka la taifa hilo. Wasimamizi wa soka ya Italia walikutana Mei 13 na kuafikiana kuhusu tarehe ya kuanza upya kwa kivumbi hicho kitakachoendeshwa chini ya kanuni mpya za afya ambazo zimetolewa na serikali ya Italia katika juhudi za kudhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya corona. Vikosi vyote 20 vya Serie A vilirejea kambini mapema Mei ila kila mchezaji anajifanyia mazoezi kivyake. Ligi Kuu ya Italia ilisimamishwa kwa muda mnamo Machi 9 zikiwa zimesalia mechi 12 zaidi za kutandazwa katika kampeni za muhula huu. Juventus ambao wanafukuzia ubingwa wa taji la Serie A kwa mara ya tisa mfululizo msimu huu wanaselelea kileleni mwa jedwali kwa alama 63, moja zaidi kuliko Lazio. Kwa mujibu wa vinara wa soka wa Italia, wanasoka wa vikosi vyote 20 vya Serie A wataanza kushiriki mazoezi ya pamoja kuanzia Jumatatu ya Mei 18, 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako